Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi akutwa ameoza ndani ya nyumba

Kifo Mauaji Wachimbaji Madini?fit=640%2C426&ssl=1 Bibi akutwa ameoza ndani ya nyumba

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: Nipashe

Bibi aliyefahamika kwa jina la Lucia Masanja (78) mkazi wa Kijiji Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga, amekutwa ndani ya nyumba yake akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umeoza.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nduguti wilayani Shinyanga Saleh Manota akizungumza kwa njia ya simu na Nipashe jana, amesema tukio hilo limetokea Novemba 3 mwaka huu.

Amesema taarifa za mwili wa bibi huyo kukutwa amefia ndani ya nyumba yake alizipata kutoka kwa wananchi na alipofika eneo la tukio nyumbani kwa bibi huyo alikuta kuna harufu kali huku mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.

Anaendelea kusimulia kuwa baada ya kuona bibi huyo amefariki, ikabidi wapige simu polisi na walipofika ikabidi wavunje mlango na kumkuta bibi huyo akiwa ameshafariki na inaonesha ni siku nyingi kwani mwili wake ulikuwa unatoa harufu kali.

“Tumemkuta bibi huyu Lucia Masanja nyumbani kwake akiwa amefariki na ameoza kabisa, inaonekana alifariki siku nyingi na wananchi wamemgundua mara baada ya kusikia harufu kali ikitoka ndani ya nyumba yake,”amesema Manota.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa yupo kwenye majukumu mengine atalitolea taarifa baadae.

Chanzo: Nipashe