Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi Harusi na mama yake mzazi wafarika katika ajali

Bibi Harusi X Mama Mzazi Bibi Harusi na mama yake mzazi wafarika katika ajali

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wamefariki dunia akiwemo Rehema Dias Chao (37) anayetajwa kuwa ndiye alikua akiendesha moja ya magari yaliyohusika katika ajali hiyo akielekea nyumbani kwao Marangu kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake.

Taarifa ya jeshi la Polisi imesema tukio Hilo limetokea Novemba 28, 2023 saa 7:00 mchana katika barabara kuu ya Moshi - Mwanga eneo la Kichwa cha Ng’ombe, Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro, ambapo gari lenye namba za usajili T.770 AHV aina ya Scania Lori lenye tela namba T.705 AHV mali ya AVCO Investment Ltd ya mkoani Arusha, likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam, liligongana na gari ndogo lenye namba za usajili T.121 CYM aina ya Toyota Raum .

Rehema Dias Chao, (37), mwalimu wa Shule ya Sekondari SUA na mkazi wa Morogoro, aliyekua akitokea Morogoro kuelekea Marangu, Moshi anatajwa kufariki dunia pamoja na abiria waliokuwa kwenye gari hilo Agnes Dias (75), mkazi wa Marangu, Moshi na Arine Shija (15), mkazi wa Geita.

Katika ajali hiyo watu wawili ambao ni Veronica Dias Chao, (35), mkazi wa Geita na Jayden Erasto (2) mkazi wa Morogoro wanejeruhiwa vibaya.

Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na kwamba Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari T.770 AHV Scania kwa mahojiano zaidi.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya Kisangara, Mwanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live