Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benki ya Exim yatoa zawadi ya Eid kwa watoto mikoa minne

Xxxxxxxxxxxxxxxx Benki ya Exim yatoa zawadi ya Eid kwa watoto mikoa minne

Wed, 12 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Lengo ni kuwawezesha watoto hao waweze kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr.

Msaada huo ulikabidhiwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwa wameambatana na wafanyakazi wengine na ulihusisha mahitaji muhimu ikiwamo mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maharage pamoja na katoni za juisi na maji ya kunywa.



Akiwasilisha msaada huo katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha New Faraja Orphanage Centre kilichopo Mburahati Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, amesema imekuwa ni utaratibu wa benki hiyo kusaidia makundi na taasisi mbalimbali kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kwa jina “Exim Cares”.





“Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr, na ni mwendelezo wa utaratibu wetu wa kile ambacho tumekuwa tukikifanya kila mwaka ambapo wafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na uongozi kwa ujumla tumekuwa tukiguswa kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi kwenye vituo hivi wanafurahia Sikukuu hizi kama wenzao waliopo majumbani,'' amesema.





Kafu amevitaja vituo vingine ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni cha watoto yatima cha Nuru kilichopo jijini Mbeya, Kituo cha Shinyanga Society kilichopo mkoani Shinyanga na Kituo cha Shalom kilichopo wilayani Karatu.

Kafu ametoa wito kwa watoto hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii huku wakitanguliza nidhamu kwenye kila jambo wanalofanya ikiwamo masomo na shughuli zao za kila siku wawapo shuleni na kituoni hapo.



Wawakilishi wa vituo hivyo wameishukuru benki hiyo kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine.
Chanzo: ippmedia.com