Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi laua watu 4 Morogoro

A90eec8ab826dffa54dc85cb57d5d3d5 Basi laua watu 4 Morogoro

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU wanne wamekufa na wengine sita wamejeruhiwa baada ya basi dogo lililokuwa likitoka Mbezi jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro kugonga tela la lori jana saa tatu asubuhi.

Basi hilo lenye namba za usajili T149 DNZ aina yaToyota Coaster liligonga tela lenye namba za ujasili T 394 DHK lililochomoka kwenye lori lenye namba za usajili T 199 EKW aina ya Scania.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la kati ya Nane Nane na seminari katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.

Tela hilo lililokuwa limeungaanishwa kwenye lori lililotoka Morogoro kwenda Dar es Salaam lilikatika kwenye maungio na kuziba barabara kuu hivyo kusababisha basi hilo ndogo liliparamie ubavuni.

Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya jana alithibitisha kupokewa watu wanne walioaga dunia kutokana na ajali hiyo na majeruhi sita.

Alisema, watatu kati ya marehemu hao ni wanaume. Dk Lyamuya , alisema kati ya majeruhi sita , mmoja ni mwanamke na kwamba, mmoja alitibiwa na kuruhusiwa, na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri ingawa wengine wamevunjia miguu na kuumia kichwani hivyo kusababisha wakose fahamu.

"Na kama itahitajika kuwahamishia kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili , hiyo itatengemea maendeleo ya hali zao" alisisitiza Dk Lyamuya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Willbroad Mutafungwa, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa tatu asubuhi katika eneo la kati ya Nane Nane na Seminari kwenye barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.

Mutafungwa , alisema Lori hilo lenye namba za usajili T 199 EKW aina ya Scania ilikuwa na tela namba T 394 DHK ikitoka Morogoro na kubeba shehena ya Tumbaku ilipofika eneo hilo tela lake lililounganishwa na lori lilikatika na kuziba barabara ya Morogoro- Dar es Salaam .

Kamanda Mutafungwa , alisema gari dogo la abiria aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitoka Dar es Salaam likiwa na abiria 10 liligonga katikati ya tela hilo.

Alisema, mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo askari Polisi na wenzao wa zimamoto na uakoaji walifika mara moja eneo la tukio kuokoa abiria.

Mutafungwa , alisema baada ya ajali hiyo walifutilia Track iliyokuwa kuwa na tela hilo na kubaiini kuwa dereva alilitekeleza mbali na ilipotokea ajali hiyo na kutoweka kusiko julikana na anaendelea kusakwa na Polisi huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kufanyika.

Alishukuru msaada uliotewa na kampuni ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kutoa mashine iliyowezesha kunyanyua basi ndogo na tela yaliyokuwa yameziba barabara.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Goodluck Zelote , alisema baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo walifika wakiwa na vifaa vya uokoaji ili kuzuia madhara yasitokee.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Pascal Mlela, alimshukuru Mungu kwa kumusuru katika ajali hiyo na kusema hajui alivyookolewa kwani alijikuta yupo nje.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare ambaye alifika eneo la tukio hilo alitumia fursa hiyo kuwaonya madereva na wamiliki wa magari kufanya ukaguzi kabla ya kuanza safari.

Chanzo: habarileo.co.tz