Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

 Basi latumbukia shimoni Bukoba,  watu nane wafariki

05d9912d5a8e61995f135c2c0273d7e2.jpeg Basi latumbukia shimoni Bukoba, watu nane wafariki

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Watu nane wamefariki dunia na wengine sita wanapatiwa matibabu katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya gari walilokuwa wanasafiria kukatika mfumo wa breki kabla ya kutumbukia shimoni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malim basi hilo dogo linalofanya safari zake Kemondo na Manispaa ya Bukoba limepata ajali katika barabara ya Uganda, Mtaa wa Rwamishenye.

Ameeleza kuwa gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T471DCG lilikuwa linatokea Kemondo na kwenda Bukoba Mjini jana.

Alisema kuwa Polisi wanamshikilia dereva wa gari hilo, Ismaili Rashid.

Chanzo: habarileo.co.tz