Basi la kampuni ya Tahmeed limeteketea kwa moto leo wakati lilipokuwa njiani likielekea Mombasa.
Basi hilo lilikuwa likielekea Mombasa kutoka jijini huku likiwa na abiria hao 42 ambao waliponea.
Walioshuhudia kisa hicho walisema mkasa ulitokea mita chache kabla ya basi hilo kufika mjini Voi.
Afisa wa polisi wa kaunti ndogo ya Voi Bernastein Shari amedhibitisha kisa hicho akisema kilifanyika saa kumi unusu jioni.
"Basi hilo l kampuni ya Tahmeed lilikuwa na abiria 42 likielekea Mombasa kutoka jijini Nairobi," alisema afisa huyo.
Abiria wote waliokolewa kabla ya ndimi za moto kumeza basi hilo lote hadi likageuka jivu.
Picha za basi hilo likiteketea ziliibuka kwenye mtandao na Wakenya kutoa hisia mseto.
"Yaani kuna watu watakimbia katika eneo la mkasa ili kurekodi tu yale ambayo yanafanyika," mmoja wa mwanamtandao alisema.