Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi la Frester laua wanafunzi wawili

Frester Dsa Basi la Frester laua wanafunzi wawili

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Kiteyagwa, waliokuwa wamepanda baiskeli wamefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Kampuni ya Frester aina ya Zhontong lenye namba T.567 DFA, ambalo hufanya safari zake kati ya Wilaya ya Karagwe na Jiji la Mwanza lililokuwa likitokea Karagwe wakati kilielekea kwenye standi kuu ya mabasi ya Bukoba.

Kamanda wa Jeshi Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishina Msaidizi, Blasius Chatanda amethibitisha juu ya tukio hilo na kusema dereva wa basi hilo anashikiliwa na jeshi hilo.

Ajali hiyo imetokea karibu na kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo katika Kata ya Kagondo iliyoko kwenye Manispaa ya Bukoba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live