Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi, Lori yagongana uso kwa uso daraja la Wami

15188 Pic+wami TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Basi la kampuni ya Kidio One na lori yamegongana uso kwa uso katika daraja la wami mkoani Pwani leo asubuhi Septemba 2, 2018.

Basi hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Arusha. Chanzo cha ajali inadaiwa ni basi hilo kufeli mfumo wa breki.

Katika tukio hilo abiria wamepata majeraha puani kwa kuvuja damu huku ikielezwa dereva naye kaumia. Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea ajali hiyo na kwamba wanafuatilia zaidi.

Tukio hilo limesababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa magari yatokayo mikoa ya Kaskazini na yanayotoka Der es Salaam kwenda huko yamekwama ili kusubiri lori na basi hilo yaondolewe darajani.

Chanzo: mwananchi.co.tz