Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa kusaini ujenzi barabara ya Kilolo Iringa

Bashungwa: Rais Samia Yupo 'serious' Na Ujenzi Wa Barabara.jpeg Bashungwa kusaini ujenzi barabara ya Kilolo Iringa

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego, leo Oktoba 05, 2023.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atashuhudia utiaji saini wa Ujenzi wa Barabara ya Ipogolo (Iringa) hadi Kilolo yenye km 33.6 kwa kiwango cha Lami na kukagua Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Iringa.

Aidha, Waziri Bashungwa atakagua Barabara ya Mchepuo ya Iringa (Eneo la Igumbilo stand na Njia panda ya Chuo Kikuu cha Iringa) pamoja na eneo la barabara katika Mlima wa Kitonga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live