Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa atoa miezi mitatu kwa DED Musoma Vijijini

Bashungwaa Ic Data Innocent Bashungwa, Waziri wa TAMISEMI

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa ametoa miezi mitatu ya uangalizi wa utendaji kazi wa mkurugenzi wa halmashauri ua Musoma Vijijini, Msongela Palela.

Bashungwa ametoa muda huo leo Jumamosi, Mei 7, 2022 baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi makao makuu pamoja na hospitali ya halmashauri hiyo miradi ambayo amedai kuwa inatekelezwa kwa kusuasua.

"Nakupa muda wa miezi mitatu ya uangalizi wa utendaji wako wa kazi nisipoona mabadiliko nitachukua hatua za kinidhamu hatuwezi kwenda kwa mwendo huu wananchi wanataka huduma nyie hamjali," amesema.

Amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo licha ya kwamba serikali imetoa fedha jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine linasababishwa na uzembe wa mkurugenzi huyo pamoja na wasaidizi wake.

"Mkurugenzi kama kuna kitu chochote kinakukwamisha, sema tuchukue hatua hata kama ni wasaidizi wako au mtu yeyote maana hatutaki kumuonea mtu na mjue kuwa tunapochukua hatua sio kwamba tunataka kumkomoa mtu hata sisi hatupendi tumbua tumbua," amesema.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri mkurugenzi huyo amesema kuwa ujenzi ulianza mwezi Aprili mwaka 2021.

Advertisement Amesema kuwa ujenzi huo ambao hivi sasa bado upo katika hatua ya msingi ulikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwepo ukosefu wa vifaa vya ujenzi kama vile mawe, kokoto na mchanga kutoka katika eneo la mradi.

Amesema kuwa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Suma JKT unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh2.7 bilioni na kwamba hadi sasa wamekwisha pokea Sh2 bilioni huku kuhusu mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya akisema kuwa tayari wamepokea Sh3.4 bilioni.

Amesema hospitali hiyo ya wilaya ilianza kujengwa mwaka 2019 ambapo majengo yake yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live