Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa atoa maagizo kwa ma DC, RC

Bashingwaaapic Bashungwa awashukia ma DC, RC

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Innocent Bashungwa amesema wizara yake itawachukulia hatua wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri watakaoshindwa kukamilisha miradi ya afya ifikapo April 30, 2022.

Pamoja na hilo Bashungwa ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Jiji la Mbeya kukamilisha miundombinu ya majengo likiwemo jengo la mama na watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Igawilo

Bashungwa ametoa agizo hilo leo Jumatano Machi 16, 2022 mkoani Mbeya alipofanya ziara katika hosptali hiyo.

Amesema amefanya ziara za kukagua miundombinu ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati nchi nzima na jiji la Mbeya ndio amehitimisha ziara hizo.

Amesema Serikali imetoa zaidi ya Sh243.9 bilioni kwa ajili ya miradi 233 huku iliyokamilika ikiwa 110 pekee.

''Kwa halmashauri ambazo hazijafanya vizuri na kukamilisha miradi kwa wakati wakuu wa wilaya, wakurugenzi watawajibishwa.

“Nitasikitishwa sana Jimbo analotoka Spika likawa ni miongoni mwa viongozi wake kuchukuliwa hatua na kuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Triphonia Kisiga kuhakikisha miradi hiyo inakwenda kwa kasi ili Mbeya ipige hatua ''amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chua chua amesema kwa maslai mapana ya Taifa watasimamia miradi yote ikamilike kwa wakati.

Amesema anatoa ahadi kabla ya Aprili 30, 2022 miradi yote ya ujenzi na ukarabati ya miundombinu katika hosptali za wilaya, vituo vya afya na Zahanati kukamilika kwa wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live