Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa afika Shinyanga kutazama athari za mvua

Bashungwa 01 Bashngwa afika Shinyanga kutazama athari za mvua

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, Desemba 8, 2023.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo pamoja na maeneo mbalimbali nchini.

Miundombinu hiyo iliyoharibiwa na mvua ni pamoja na barabara ya Shinyanga - Old Shinyanga, barabara ya Old Shinyanga - Solwa, barabara ya Solwa - Kahama na miundombinu mingine ya barabara katika mkoa huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live