Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Barua za Mapenzi" chanzo mimba za utotoni

Mimba Ed "Barua za Mapenzi" chanzo mimba za utotoni

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na Nipashe diwani wa kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Joseph Kabadi anaeleza kuwa kipindi cha nyuma watoto wengi walibebeshwa ujauzito na kutatisha masomo yao lakini kwa kiasi kikubwa  walifanikiwa kupunguza tatizo hilo.

Anaeleza kuwa kwa sasa kesi zilizopo nyingi ni watoto wa kike hasa wanafunzi kukamatwa na barua za kimapenzi jambo ambalo linahatarisha ustawi wa mtoto na kuchangia upatikanaji wa mimba  zisizotarajiwa.

Aidha anaeleza tatizo ilo linachangiwa na baadhi ya watu  kupenda kuwarubuni watoto hasa waliopo mashuleni jambo ambalo ni hatari na lenye kurudisha maendeleo nyuma.

" Tunapokea sana kesi hizo hazipiti siku malalamiko yaleyale yanajirudia vijana wengi wanajihusisha na masuala ya mapenzi hasa bodaboda wanatajwa sana ndio wanawaandiikia barua na kuharibu maisha ya watoto wetu wazazi wawe makini pia wajenge tabia ya kuwakagua mara kwa mara kuwapa elimu ya afya ya uzazi ,namna ya kujilinda Ili waweze kutimiza ndoto zao " alieleza Kabadi.

Aidha akizungumzia ujenzi unaendeleaje wa kituo cha afya cha Bulale kilichopo kwenye kata yake kitakacho gharimu millioni 250 anaeleza kuwa kituo hicho kitawanusuru akinamama waliokuwa wakifuata huduma mbali pia elimu ya afya ya uzazi itakayotolewa itawasaidia hasa vijana.

Chanzo: ippmedia.com