Mon, 19 Jun 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Hali ya kuwepo kwa baridi kali mikoa ya nyanda za juu iliyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA wiki mbili zilizopita sasa imeanza kujitokeza kufuatia baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya baridi lake kufikia nyuzi joto Saba.
Utabiri wa saa 24 uliotolewa na TMA unaonesha kuwa uwepo huo wa baridi kali katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo yanaweza kuendelea huku baadhi ya maeneo yakiwa na joto la nyuzijoto 25.
Mkoa wa Njombe wenyewe unafuatia kwa kuwa na baridi kali kutokana na utabiri huo kuonesha uwepo wa baridi inayofikia nyuzi joto 8.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live