Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza la Madiwani Namtumbo lamkataa Mkurugenzi

Baraza La Madiwani Namtumbo Lamkataa Mkurugenzi.jpeg Baraza la Madiwani Namtumbo lamkataa Mkurugenzi

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Madiwani Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma limemkataa Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Chiriku Chilumba kufanya kazi katika Halmashauri hiyo kwa madai ya kutotekeleza Majukumu yake kikamilifu na kuwasimamisha kazi wakuu wa idara watatu kutokana na Ubadhirifu wa Fedha.

Maazimio hayo yamesomwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Juma Pandu baada ya baraza kugeuka kamati ambapo lilimalizika usiku na lilikuwa na mvutano Mkali

Wakuu wa idara waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni Afisa manunuzi wa Halmashauri Wille Ndabila, Mganga mkuu wa Halmashauri Dkt. Arron Hyera na Afisa Elimu wa Sekondari Michael lyambilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live