Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara ya njia nne kupunguza ajali Bukoba

Barabara 373446391 Barabara ya njia nne kupunguza ajali Bukoba

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema kuwa wananchi wa Manispaa ya Bukoba wanakwenda kuondokana na changamoto ajali ambazo zimekuwa zinagharimu maisha ya watanzania wengi kutokana na mteremko mkali na kona ya Nyangoye mjini Bukoba.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa Barabara hiyo unaoendelea ambapo awamu ya kwanza Barabara hiyo itajengwa kilometer 1 kutoka Rwamishenye hadi mtaa wa Mitaga kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 4.6.

Sambamba na hayo amewataka wananchi ambao nyumba zao zinaguswa na mradi wa Barabara ya njia 4 inayotoka Rwamishenye hadi bandari ya Bukoba wanaodai fidia ya shilingi bilioni 1.8 kuendelea kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendale kuratibu zoezi hilo la kuwalipa fidia.

Mtuli Mwaikokesya ni meneja wa wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Kagera ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 25 huku Hamimu Mahmudu akiipongeza serikali kwa niaba ya CCM Kwa namna unavyotekeleza ilani ya uchaguzi mkoani Kagera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live