Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara ya Mtwara-Masasi kukamilika Januari, 2019

26643 Pic+barabara TanzaniaWeb

Tue, 13 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imepanga kujenga kwa awamu barabara ya Mtwara- Newala-Masasi ambapo sehemu ya kwanza ujenzi ulianza April 17, 2017 na unategemea kukamilika Januari mwaka 2019.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eliasi Kwandikwa amesema bungeni leo Jumatatu Novemba 12, 2018 kuwa kipande walichoanza nacho ni Mtwara-Mnivata chenye urefu wa kilomita 50 ambayo itagharimu Sh89.6 bilioni.

Katika swali la msingi, Abdallah Chikota (Nanyamba-CCM) ametaka kujua ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza ili kuwaondolea kero wananchi wa maeneo hayo.

Naibu waziri amesema Serikali inaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo katika mwaka 2018/19 Serikali imetenga Sh10 bilioni.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri kipande cha barabara iliyobaki ya kuanzia Mnivata -Newala hadi Masasi yenye urefu wa kilomita 60 kitajengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mwisho,.....



Chanzo: mwananchi.co.tz