Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara ya Morogoro yafunguliwa baada ya kufungwa kwa saa sita

56124 Barabarapic

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Barabara ya Morogoro jijini hapa imefunguliwa leo mchana Jumanne Mei 7, 2019 baada ya kufungwa kwa zaidi ya saa sita kutokana na kujaa maji yaliyotokana mvua kubwa inayonyesha tangu juzi.

Barabara hiyo ilifungwa leo asubuhi eneo la Jangwani kutokana na kuja maji na kutopitika.

Akizungumza na Mwananchi leo Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es Salaam (ZTO), Matson Mwakyoma amesema wamefungua barabara hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kila kitu kipo sawa na magari yanaweza kupita.

Awali,  Mwakyoma alibainisha kuwa walifunga kipande hicho cha barabara ya Morogoro kutokana na kujaa maji.

"Kwa kawaida huwa tunapima vitu vingi, unaweza kuona maji yamepungua lakini hatujafungua kwa sababu tunaangalia kama tope lilipo gari zinaweza kupita,”

"Kabla ya kufungwa ndiyo maana gari zetu zimekuwa zikipita mara kwa mara kufanya ukaguzi, kujiridhisha kuwa kila kitu nipo sawa, tumefungua baada ya kuona hakuna madhara" amesema Mwakyoma.

Kwa upande wa Deus Bugaywa mkuu wa idara ya mawasiliano kampuni ya Udart amesema kuwa mipango ya kuhamisha ofisi ikiwamo maegesho ya magari kwenye eneo hilo inaendelea kufanyiwa kazi.

Miongoni mwa waathirika wa eneo hilo kujaa maji ni mabasi ya mwendokasi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz