Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara ya Makambako, Njombe - Ruvuma kujengwa

Lami Barabaraaaa Barabara ya Makambako, Njombe - Ruvuma kujengwa

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeanza kukarabati kwa kiwango cha lami barabara ya Makambako, Njombe hadi Ruvuma yenye urefu wa kilomita 295. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi na kukuza uchumi kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Njombe, Mhandisi Ruth Shalluah wakati akizungumza mafanikio ya wakala huo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya barabara.

Amesema Serikali kupita wakala huo imeendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo Barabara ya Itoni, Ludewa hadi Manda yenye urefu wa kilomita 211.42 huku sehemu ya kwanza kutoka Itoni hadi Lusitu (kilomita 50) kwa kiwango cha zege ambapo ujenzi unaendelea.

"Ujenzi wa sehemu ya pili ya Lusitu hadi Mawengi (kilomita 50) kwa kiwango cha zege la saruji ambapo, mradi huo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 98 huku mkandarasi akiendelea kukamilisha kazi ndogondogo ikiwemo kupanda nyasi, uwekaji wa alama za barabarani na ujenzi wa matoleo ya barabara," amebainisha.

Ameongeza kuwa ujenzi wa Barabara ya Isyonje, Kikondo hadi Makete (kilomita 92.6) kwa kiwango cha lami na zege kuanzia Kitulo kwenda Iniho (kilomita 36.3) na mizani kwenye Kijiji cha Igagala unaendelea.

Pia, Mhandisi Shalluah ameeleza ujenzi wa Barabara ya Njombe hadi Makete (kilomita 107.4) kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 100, na tayari Serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami katika Barabara ya Chimala, Matamba hadi Kitulo.

Pia, Barabara ya Mkiu, Liganga, Madaba (kilomita 112), Barabara ya Njombe (Kibena), Lupembe, Madeke (Mfuji – Morogoro / Njombe Border (kilomita 125) na Barabara ya Bulongwa, Madihani, Kidope (kilomita 22.15).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live