Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara ya Kibada- Mwasonga kuwekewa lami

Bashungwa Mvua Kibada (600 X 349) Barabara ya Kibada- Mwasonga kuwekewa lami

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali tayari imeshampata Mkandarasi na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 kwa kiwango cha lami.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongezwa kwa ujenzi wa kilometa 10 katika barabara hiyo ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji kwa kuinganisha na kipande kilichobakia cha Kimbiji hadi Cheka kwa kiwango cha lami.

Bashungwa amezungumza hayo Aprili 29, 2024 Wilayani Kigamboni Mkoani Dar es Salaam katika ziara yake ya kikazi ya kukagua athari za miundombinu ya barabara na madaraja zilizotokana na mvua za El-Nino na kujionea hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Serikali iko kazini na imejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TANROADS na TARURA kurekebisha maeneo yote yaliyopata athari ili ziendelee kupitika na kutokwamisha shughuli za wananchi na viwanda katika uzalishaji.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameeleza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam hauna mafuriko ila wananchi wameziba njia za maji kwa kujenga nyumba kwenye mikondo ya maji na kusistiza kuwa Mkoa huo unahitaji kufumuliwa upya kwa na kujenga mifereji imara ya maji ya mvua ili kuzuia maji kutoingia kwenye makazi ya wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live