Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara Mtwara –Tunduru yatengewa bil 2.2/-

7c17294e29b585d01bf1b23574edf601 Barabara Mtwara –Tunduru yatengewa bil 2.2/-

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi katika Mwaka wa Fedha 2020/21, imetenga Sh bilioni 2.293 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara ya Mtwara hadi Tunduru.

Kauli hiyo ilitolewa Bungeni jana na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate (CCM).

Mpakate alitaka kujua ni lini barabara ya Mtwarapachani– Nalasi – Tunduru itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri Kasekenya alisema, wizara hiyo kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), imekamilisha upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mtwarapachani– Lingusenguse – Nalasi Tunduru yenye urefu wa kilometa 300 kwa kiwango cha lami.

"Kazi hii ilitekelezwa na mhandisi Mshauri M/s GEG wa Ureno kwa gharama ya Sh bilioni 2.559 na ilikamilika mwaka 2020. Serikali inatafuta fedha ili kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami," alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz