Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara 16 Musoma Vijijini kulamba bilioni mbili za tozo

ROAD Barabara 16 Musoma Vijijini kulamba bilioni mbili za tozo

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

SHILINGI bilioni mbili zinazotokana na tozo mbalimbali zikiwamo za simu na mafuta, zinatarajiwa kutumika katika ujenzi na uboreshaji wa barabara 16 za ndani ya jimbo la Musoma Vijijini, wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Baadhi ya barabara ni za vijiji vya Mmahare, Etaro, Nyasaungu, Mugango, Bwai, Kwitururu, Kwikuba, Bwai Kumsoma, Maneke, Mayani, Kyawazaru, Nyaminya, Kataryo, Rwanga, Seka, Mikuyu, Saragana na Nyambono.

Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) wa wilaya hiyo, Mhandisi Hussein Ibrahim, ametaja vijiji vingine ambavyo barabara zake zitafaidika na fedha za tozo kuwa ni Chumwi, Kaburabura, Masinono na Bugwema.

"Tunatarajia kujenga na kuboresha barabara 16 kwa kutumia fedha za tozo kutoka serikali kuu, kwa sasa tunaendelea na maandalizi ili mara tu tutakapozipokea, kazi ianze mara moja," amesema Mhandisi Hussein.

Mbunge wa Musoam Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ambaye barabara hizo ziko jimboni mwake, amewaomba wananchi wasaidie uparikanaji wa molamu ili ujenzi utakapoanza, ufanyike kwa haraka.

"Ni muhimu wananchi watoe ushirikiano kadri inavyowezekana wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara za vijijini mwetu ili kazi itakapoanza, ikamilike haraka," Prof. Muhongo amesema.

Aidha, mbunge huyo ameishukuru serikali kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara za jimbo lake ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Chanzo: ippmedia.com