Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangi, mirungi yatikisa wanafunzi Kilimanjaro

Images (7) Mirungi Kenya.jpeg Bangi, mirungi yatikisa wanafunzi Kilimanjaro

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi unazidi kutikisa mkoani Kilimanjaro baada ya wanafunzi tisa wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Sanyajuu wilayani Siha wakihusishwa na kukutwa na misokoto ya bangi.

Matukio ya aina hii si mara ya kwanza kutokea kwani mwaka jana wanafunzi 10 wa Shule ya Sekondari ya Anna Mkapa katika Manispaa ya Moshi walisimamishwa masomo kwa tuhuma za uvutaji bangi huku mmoja wao akijihusisha na biashara hiyo shuleni.

Vilevile, mwaka 2020 wanafunzi wengine tisa wa shule hiyo walisimamishwa masomo baadaye bodi ya shule ikaamua wapewe nafasi nyingine kwa wazazi kuwatafutia shule nyingine, ili kuvunja makundi mabaya waliyokuwa nayo.

Kana kwamba haitoshi, kumekuwepo na taarifa za wanafunzi katika shule nyingine ndani na nje ya Manispaa ya Moshi wanaojihusisha na ulaji wa mirungi.

Akizungumzia tukio la wanafunzi wa Sekondari ya Sanyajuu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alithibitisha kukamatwa kwao saa 1:30 asubuhi Oktoba 11, mwaka huu.

Kamanda alieleza kuwa, mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 16, ndiye aliyekamatwa akiwa na bangi hiyo na simu janja aina ya Samsung mfukoni kwake, na katika mahojiano alikiri kukutwa na bangi ambayo aldai amepewa na kijana mmoja kwa ajili ya kuiuza.

Alidai pia amepewa simu hiyo kwa ajili ya mawasiliano.

Kamanda Maigwa alisema, siku ya tukio, mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo alibaini baadhi ya wanafunzi kutokuwepo mstarini na alipofuatilia akawakuta wakiwa wamejificha huku mmoja wao akiwa na bangi mfukoni.

“Baada ya kufuatilia aliwakuta hao tisa wakiwa wamejificha pembeni ya jiko la shule, ambapo aliwataka waruke kichurachura kuelekea mstarini na wakati wanaruka mmoja alikuwa ameweka mkono mfukoni.

“Kitendo cha kuruka huku ameweka mkono mfukoni, kilimtia shaka mwalimu, na alipompekua akamkuta na kete nne za bangi na simu.

Mwalimu alitoa taarifa kwa mkaguzi wa polisi wa eneo hilo ambaye alifika na kumkamata mwanafunzi huyo na wenzake wanane na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano,” alisema.

Kamanda alisema katika mahojiano mwanafunzi huo alikiri kukutwa na bangi ambayo alidai kupewa na kijana mmoja kwa ajili ya kwenda kuiuza.

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumtafuta mhusika, lakini kimsingi kesi hii itamkuta mwanafunzi huyu mmoja aliyekiri,” alieleza.

“Tayari wote wamehojiwa, katika uchunguzi huu, tutafuatilia kubaini kama wanafunzi hao wengine wanajihusisha na matumizi ya bangi na kubaini wahusika wengine wanaofanya biashara hii kwa kuwatumia wanafunzi huyo,” alisema.

Ndugu wa mmoja wa wanafunnzi waliokamatwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, mkazi wa Sanya juu, alieleza kuwa, siku ya tukio alipigiwa simu na mwalimu wa shule hiyo, afike shuleni na alipofika alimkuta mdogo wake yupo katika foleni ya wanafunzi waliokamatwa na misokoto ya bangi.

Chanzo: mwanachidigital