Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari ya Dar kuanza kutoa huduma kidijitali

Thu, 5 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ili kuboresha zaidi huduma zake, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itaanza kutoa huduma za kidijitali kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi.

Hayo yalibainishwa jana wakati wa kongamano la wadau wa ndani na nje wanaotumia bandari nchini lililofanyika jijini hapa mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye.

Akizungumza katika kongamano hilo, mkurugenzi wa TPA, Deusdedit Kakoko aliwahakikishia watumiaji bandari kuwa maboresho mbalimbali yanafanyika na yataendelea ili kurahisisha utoaji wa huduma.

Naye Waziri wa Usafirishaji Jimbo la Kivu nchini DRC, Jeon de Dion alisema changamoto zinazolalamikiwa na wafanyabiashara nchini mwake wanaotumia bandari hiyo ni mizigo kusubiri muda mrefu na ushuru wa bandari.

“Wanalalamikia zaidi gharama za matumizi ya bandari ni kubwa, lakini zaidi ni changamoto ya kuchelewa mizigo kwa siku 15. Wanaomba mambo hayo yatazamwe upya ili kuweka unafuu kwao,” alisema Dion.

Awali, akifungua kongamano hilo Nditiye alisema Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.

“Hivi sasa sheria hairuhusu ubia na sekta binafsi katika huduma za reli, lakini tunatarajia kufanya marekebisho ili uwepo ushirikiano katika baadhi ya mambo,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz