Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bandari Tanga wavuka ukusanyaji wa fedha

F6b093032bc2bc206cbb6314a9a527e2.jpeg Bandari Tanga wavuka ukusanyaji wa fedha

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Bandari mkoani Tanga imevuka lengo la makusanyo yake ya mapato na kuhudumia mizigo katika bandari kwa mwezi Mei mwaka huu, kwa kukusanya Sh bilioni 4.4 wakati lengo ilikuwa ni kukusanya Sh bilioni 2.6.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Donald Ngaile, alibainisha hayo wakati akitoa taarifa ya ufanisi wa utendaji kazi kwa waandishi wa habari juzi katika Maonesho ya Biashara na Utalii yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako jijini Tanga.

Ngaile alisema mafanikio hayo yanatokana na maboresho makubwa ya kimiundombinu yaliyofanywa na serikali ikiwemo uwepo wa vifaa vya kisasa vya kupakulia shehena za mizigo.

"Kwa upande wa mapato, tumevuka malengo tuliyoyaweka, tulitarajia kukusanya Sh bilioni 2.6 lakini tumekusanya Sh bilioni 4.4.”

“Hii inatupa mwanga kuwa, sasa bandari hii inakwenda kufungua milango ya biashara mkoani hapa na nchi kwa jumla," alisema Ngaile.

Kuhusu kuhudumia shehena ya mizigo, alisema walikadiria kuhudumia mizigo na bidhaa nyingine zinazopitishwa bandarini kwa mwezi Mei tani 120,000, lakini wamekivuka kiasi hicho hadi kufika tani 125,677.

Aliwataka wananchi wa Tanga kuendelee kuitumia Bandari ya Tanga ili iendelee kuwa na tija kwa taifa na kwa wananchi wa mkoa huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz