Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi wa Usalama afariki kwa kugongwa na basi la shule

AJALI GLORY Glory Laurent enzi za uhai wake

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi Glory Laurent wa Shule ya Msingi Karanga mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye alifariki dunia kwa kugongwa na gari la shule ameagwa rasmi na kuzikwa nyumbani kwao Rombo jana Jumanne, Aprili 26, 2022.

Glory ambaye pia alikuwa Balozu wa Usalama Barabarani katika program ya Junior Road Safety Ambasasador alifariki kwa Kugongwa na Bus la Shule baada ya kuanguka barabarani kutoka kwenye baiskeli aliyokuwa amepanda wakiekelea shuleni.

Taarifa kuhusu tukio hilo zinaeleza kuwa, chanzo ni basikeli hiyo kuyumba baada ya kugongwa na bodaboda ndipo alianguka na kugongwa na basi hilo Aprili 21, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live