Mwanza. Balozi Paul Ndobho amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa akitibiwa.
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Professa Sospeter Mhongo ambaye ni mtu wa karibu na familia ya Balozi Ndobho amelieleza Mwananchi leo Jumatatu Septemba 9, 2019 kuwa mwanadiplomasia huyo amefariki jana Jumapili.
"Ni kweli Balozi (Ndobho) amefariki dunia, familia imeniruhusu kuujulisha umma lakini taarifa zaidi familia itaongea yenyewe kwa sasa bado wanajipanga," amesema Professa Mhongo
Hata hivyo alipotafutwa Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Lucy Mogele amesema, 'ngoja nifuatilie kwa undani kupata taarifa hizo nilikuwa sijazipata."
Balozi amewahi kuwa mbunge wa Musoma Vijijini kati ya mwaka 1995 na 2000 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi.