Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bajaji zasababisha mgomo wa daladala Morogoro

22463 MGOMO+PIC TanzaniaWeb

Wed, 17 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Madereva wa daladala zinatoa huduma ya usafirishaji ndani ya Manispaa ya Morogoro wamesitisha kutoa huduma ya usafiri kutokana na bajaj kufanya kazi zinazofanywa na daladala hizo.

Hali hiyo imesababisha adha ya usafiri na mfumo wa bei kati ya Sh1,000 hadi Sh6,000 kwa abiria baada ya kutokea kwa mgomo huo ulioanza saa 12 asubuhi leo Jumatatu Oktoba 15, 2018.

Bei za kawaida huwa ni Sh400 na Sh600 kwa baadhi ya maeneo huku mgomo huo ukiwanufaisha zaidi wenye bajaj, gari ndogo aina ya kenta na Toyota Noah.

Akizungumza na madereva na makondakta stendi kuu ya daladala mkoani hapa, Katibu wa Madereva wa daladala Kihonda Mjini, Daud Balali amesema madereva wamesitisha kutoa huduma ya usafirishaji kwa kurudisha magari kwa wamiliki ili suala lao lipatiwe ufumbuzi na serikali.

Amesema madereva wa bajaj wamekuwa wakichukua majukumu ya kupakia abiria stendi tofauti na matakwa ya sheria na kufanya madereva wa daladala kukosa abiria hali inasababisha ugumu wa kazi.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Morogoro wakiwamo wanafunzi wamesema mgomo huo unaleta adha ya usafiri.

Mwanafunzi wa darasa la sita, Veronica Aloyce amesema wamelazimika kutembea umbali mrefu baada ya mgomo huo.

Hata hivyo, mgomo huo umeisha mchana huu na huduma zimerejea kama kawaida.

 

Endelea  kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz