Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bahari yatishia uhai wa kisima cha gesi, mitambo yake

Wed, 5 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Kutokana na kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay Msimbati mkoani Mtwara kuendelea kumomonyoka siku hadi siku kuelekea nchi kavu,  huenda nchi ikajikuta gizani kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 4, 2018 na Naibu mkurugenzi wa Kampuni ya Maurel & Prom Tanzania inayohusika na kuchimba gesi, Elias Kilembe kwa Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alipotembelea visima hivyo vya  gesi.

Kilembe amesema  siku hadi siku bahari inasogea nchi kavu kuelekea kilipo moja ya kisima cha gesi na mitambo hali inayowapa wasiwasi.

“Hata mwaka jana ulitokea mmomonyoko lakini haukuwa tishio kama wa mwaka 2015, lakini ukija hapa baharini unakuta mchanga umeondoka wote na kupotea, kweli ni tishio kwa kambi hii,” amesema Kilembe.

Waziri wa nishati, Dk Kalemani amesema hali halisi inaonekana na hakuna haja ya utafiti, bali kinachotakiwa kufanyika ni kujengwa kwa ukuta haraka ambao utatenganisha kisima  kilipo na bahari ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

“Kuanzia sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahala mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika huku, ni vizuri kuanza sasa ili msije kukumbwa na dhoruba kubwa, haya ni maagizo ya haraka haraka wala si jambo la kufanya utafiti,” amesema Dk Kalemani.

Wakazi wa Msimbati wameishauri Serikali kuhamisha mitambo hiyo ili kuondokana na athari zinazoweza kujitokeza baadaye.

“Wangefanya utaratibu wakahamishia eneo lingine kwa sababu kama ikitokea athari yoyote pale hata sisi hatutakuwa salama,”amesema Issa Mkumba.



Chanzo: mwananchi.co.tz