Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu wa miaka 80 adaiwa kumbaka mjukuu wake wa miaka 8

RPC MAGOMI Bn Kamanda Magomi

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Luhende Tugwa (80), mkazi wa Kijji cha Ihapa Kata ya Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye miaka minane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano, Februari 8, 2023 majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya mtoto huyo kutoka shule.

Kamanda Magomi amesema kuwa, siku ya tukio mke wa mzee huyo alikuwa shamba na ndipo mzee huyo alipotumia nafasi hiyo kutekeleza unyama huo.

Kamanda Janeth amesema kuwa wanamshikilia mzee huyo kwa hatua zaidi za kisheria ili kujibu tuhuma zinazomkabili,huku akiitaka jamii kuendelea kukemea vitendo vya ukatili na kuwafichuwa watu wanaoendelea kufanya ukatili kwa wanawake na watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live