Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba, mama na mtoto wauawa kikatili

Sat, 15 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watu watatu wa familia moja wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi huku miili yao ikionyesha kuwa wamechinjwa.

Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Mayamaya kitongoji cha Zamahelo limethibitishwa na ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Grace Mwikola. 

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 13, 2018 amesema wamebaini mauaji hayo leo asubuhi baada ya watoto wa marehemu kurejea nyumbani asubuhi kutoka mahali walipokuwa wamelala.

Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Daudi Isaya na mkewe, Hilda Mazengo na mtoto wao mchanga.

“Leo asubuhi tumepokea taarifa hizo kutoka kwa watoto wakubwa wa marehemu ambao hulala nyumba ya jirani. Waliporejea asubuhi walikuta mlango uko wazi na walipoingia ndani walikuta miili ya wazazi wao na mdogo wao,” amesema.

Amesema chanzo cha vifo hivyo hakijajulikana na kwamba polisi walifika eneo hilo na kuchukua miili hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz