Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita limefanikiwa kuokoa mwili wa kichanga cha siku nne kilichokuwa kimetupwa na baba mzazi wa kichanga hicho kwenye dampo la takataka majira ya saa tatu asubuhi ya jana Januari 4/2023
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema baba wa kichanga hicho alifika na boksi likiwa na mwili na kulitupa kwenye dampo la takataka na kukimbia
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Geita Dokta Pascalates Mujuni anasema walimpokea mama wa kichanga hicho anayefahamika kwa jina la Emmanuelina Melikioli, Desemba 31, saa 10 jioni kama rufaa kutoka hospitali ya wilaya ya Nzera akiwa na tatizo la kupungukiwa Damu na mtoto kutocheza tumboni kwa siku tatu
Ameeleza kuwa ilipofika saa 1 usiku mama huyo alijifungua kwa njia ya kawaida mtoto akiwa amefariki ma hadi sasa mama wa kichanga hicho bado anapatiwa matibabu
Muda mchache baada ya baba wa mtoto kutupa mwili wa kichanga hicho jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kufika na kuuchukua mwili huo na kuurudisha hospitali kwa ajili ya taratibu za mazishi