Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba amchoma moto mwanae kisa kudokoa dagaa

Moto Msdd.jpeg Baba amchoma moto mwanae kisa kudokoa dagaa

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Grace Mwita (5), mkazi wa mtaa wa Starehe wilayani Tarime mkoani Mara amechomwa moto mikono na baba yake na kusababishiwa maumivu na majeraha makubwa akidaiwa kudokoa mboga (dagaa alimaarufu kwa jina la Furu) iliyokuwa imepikwa na baba yake mzazi kwa ajili ya chakula cha mchana.

Tukio hilo la kikatili limetokea usiku wa kuamkia leo, Novemba 28, 2023 ambapo baba wa motto huyo Mwita Abdala, amekiri kufanya tukio hilo la kumchoma moto mikono motto wake kisa alidokoa mboga.

Nao baadhi ya ananchi wa mtaa huo wameomba serikali iweze kumchukulia hatua kali za kisheria bab huyo ili wengine waweze kujifunza na wasijaribu kutekeleza tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live