Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba alawiti watoto, mke amkingia kifua

Pingu 1140x640 Baba alawiti watoto, mke amkingia kifua

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Morogoro wanamshikilia Hamad Kapera (20) mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuwanajisi watoto wake mapacha wenye umri wa miaka miwili na kuwaambukiza magonjwa ya zinaa.

Tukio hilo la kikatili linadaiwa kutokea Mei 21, 2024 wakati mama wa mapacha hao alipokwenda shambani na kuwaacha watoto nyumbani wakiwa na baba yao.

Inaelezwa kuwa mama wa mapacha hao (jina limehifadhiwa) alienda ofisini kwa Mkuu wa Wilaya Shaka Hamdu Shaka kuomba mume wake ambaye anashikiliwa asamehewe wakaendelee kulea watoto wao.

Aidha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema wanamshikilia pia mama wa watoto hao kwa kosa la kukataa kutoa ushahidi kuhusu tukio hilo na kwamba ataachiwa tu atakapotoa ushahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live