Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada

IMG 20230728 WA0070 Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa. View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine. View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE “Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live