Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumbaka mwanaye wa miaka 11

Baba Abaka 11 Baba adaiwa kumbaka mwanaye wa miaka 11

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linamtafuta mkazi wa Kata ya Magugu wilayani Babati, Frednand Yohana ambaye anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Benjamin Kuzaga ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 13, 2021 mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Kuzaga amesema mkazi huyo wa Magugu alikuwa anambaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 (jina lake linahifadhiwa) usiku wakati mke wake na watoto wengine wakiwa wamelala.

Amesema tukio hilo limefanyika kwa vipindi tofauti na lilibainika Desemba 6 mwaka huu baada ya mkewe kutoa taarifa Kituo cha Polisi Magugu.

Amesema taarifa za tukio hilo zimetolewa na mke wake, Justina Emmanuel ambapo mtoto huyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo tangu mwezi Oktoba mwaka huu.

"Walikuwa wanaishi kwenye chumba kimoja mume, mke na watoto wao watatu na uchunguzi umeonyesha Yohana amembaka mtoto wake zaidi ya mara nne," amesema Kamanda Kuziga.

Amesema mtuhumiwa alitoroka baada ya mkewe kubaini kitendo hicho na polisi wanamtafuta ili afikishwe mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live