Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba: Tumewazika watoto, wahusika waadhibiwe

Watoto Kuzikwa Kuzikwa (600 X 258) Baba: Tumewazika watoto, wahusika waadhibiwe

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Isaka Rafael (27), Baba wa Watoto mapacha waliozaliwa kabla ya wakati na mmoja wao kunyofolewa jicho na ngozi ya paji la uso wakiwa Kituo cha Afya Kaliua, amesema tayari miili ya Watoto wake imezikwa lakini ameiomba Serikali kusimamia haki ya Watoto wake Mahakamani na kuhakikisha kila aliyehusika anapata adhabu inayostahili.

Isaka ameishukuru pia Serikali, Wadau na Wananachi wote kwa ushirikiano alioupata tangu sakata hilo lilipoibuliwa.

Miili ya Watoto hao mapacha waliozaliwa kabla ya wakati imezikwa kimila nyumbani kwao (ndani ya nyumba) katika Kijiji cha Kalemela Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Kwa upande wake RC Tabora ameendelea kusisitiza kuwa Wauguzi wanne wa Kituo cha Afya Kaliua watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili wakati wowote kuanzia sasa kuhusiana na sakata hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live