Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Majaliwa afungukia hela alizopata mwanaye

Story Za Town  1667998190863 Baba Majaliwa afungukia hela alizopata mwanaye

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: RaiaMwema

Baba mzazi wa kijana Majaliwa Jackson aliyesaidia kuokoa maisha ya waliopata ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka majini Jumapili iliyopita Bukoba.

"Nilivyosema Majaliwa ni mwanangu watu walibisha, kinachoingia katika familia ni cha familia.

"Mimi na Mama Majaliwa tumetengana kwenye mambo ya ndoa lakini tupo pamoja sana hayupo mbali na mimi na mimi sipo mbali naye kwenye masuala ya familia tunashirikiana kupanga mambo ya familia" - Jackson Majaliwa ameimbia Clouds FM

Kuhusu zawadi alizopewa kijana wao huyo kwa kuvunja mlango kuokoa waliotumbukia na ndege ziwa Victoria, amesema

"Anachokipata tungeshirikiana mimi na familia kama ni kuiweka pesa yake aikute wakati anaendela kukua , tutaangalia kipi tumuhifadhie kwa sababu bado ana wadogo zake na sisi wazazi wake maisha yetu ni ya kawaida sana

"kikubwa tungemuwekea yeye kidogo tungeona namna ya kuwasaidia wadogo zake maana kinachoingia katika familia ni kwa ajili ya familia" - Baba mzazi wa Majaliwa akiongea na Clouds FM.

Chanzo: RaiaMwema