Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya bomoabomoa, ujenzi waanza Kimara

12005 Pic+bomoa TanzaniaWeb

Wed, 15 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mradi wa ujenzi wa njia ya sita katika Barabara ya Morogoro umeanza kutekelezwa.

Hata hivyo, licha ya Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama kuthibitisha kuanza kwake, hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo.

Mwandishi wetu aliyetembelea eneo la Kimara kuanzia Mwisho hadi Kibamba, alishuhudia ujenzi mkubwa ukiendelea upande mmoja.

Katika eneo la Kimara Stop Over hadi Mbezi kwa Musu-guri, alishuhudia shughuli kadhaa za ujenzi zikiendelea iki-wamo utengenezaji wa njia za dharura na usawazishaji wa vifusi.

Pia, wataalamu walionekana wakichora michoro na kuwe-ka alama katika maeneo ya ujenzi zikiwamo zinazowataka madereva kupunguza mwendo.

Katika eneo la Kimara Stop Over, maandalizi ya kuwekwa kituo cha uendeshaji wa shughuli za mradi yalionekana ya-kiendelea. Kituo hicho kimejengwa kwa kutumia kontena. Kingine kama hicho kipo Kibamba.

Taarifa kutoka Tanroads zinasema mradi huo ulianza ku-tekelezwa Agosti na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 29 (miaka miwili na miezi mitano) na kwamba utakwenda hadi Chalinze.

Ndyamukama licha ya kusema ujenzi huo umeanza al-imwelekeza mwandishi kwenda Tanroads makao makuu kwa ufafanuzi zaidi.

Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Tanroads, Aisha Malima alipotafutwa juzi alimtaka mwandishi kuuliza maswali kwa maandishi ambayo bado hayajajibiwa.

Takriban nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya eneo la mita 121.5 la hifadhi ya barabara hiyo kuanzia Kimara hadi Ki-luvya zilibomolewa kupisha mradi huo kazi iliyofanyika kuanzia Julai 8, 2017 na kukamilika Desemba mwaka jana.

Fursa na changamoto

Ujenzi huo umefungua fursa ya biashara kwa mama lishe wanaouza chakula asubuhi na mchana.

Katika maeneo hayo pia wapo wafanyabiashara ndogon-dogo (machinga) ambao wamekuwa wakipanga biashara zao katika maeneo ambayo kazi za ujenzi zimekuwa zikiendelea.

“Ujenzi umeanza lakini changamoto iliyopo ni kwamba hakuna taarifa zozote juu ya uendeshwaji wa mradi, tunaona tu makandarasi wapo kazini na hakuna taarifa zozote kwa wananchi juu ya nini kinachoendelea,” alisema Jumanne Yusuph, mkazi wa Kimara.

Tunaona kuna makandarasi Kibamba wanakuja huku Stop Over na wengine wanaanzia hapa Stop Over wanakwenda Kibamba,” alisema Hadija Hamis mkazi wa Kimara.

Chanzo: mwananchi.co.tz