Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Nahodha wa MV. Kigamboni kupigwa, DC Nyangasa afanya maamuzi haya

Mv Kigamboni MV Kigamboni

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa za kudaiwa kuvamiwa na kupigwa kwa Nahodha wa Kivuko cha MV. Kigamboni, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatuma Nyangasa na TAMESA leo wametangaza kuondolewa kazini kwa Watumishi watatu.

DC Nyangasa ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kufanya ziara ya kukagua zoezi la ukarabati wa Kivuko cha Mv. Kazi kinachofanyiwa marekebisho na Kampuni ya Songoro Marine.

"Wiki iliyopita baada ya lile tukio la ucheleweshwaji wa abiria na kusababisha abiria mmoja kutaka kuingia kwenye chumba cha Nahodha, nilitoa muda wa saa 24 ili nipewe taarifa ya nini hasa kilichotokea lakini nifahamu Wahusika waliokuwepo zamu siku ya tukio lakini pia nifahamishwe taarifa sahihi ya hatua stahiki zilizochukuliwa dhidi ya wale wote ambao walihusika kwenye changamoto hiyo,” amesema DC Nyangassa.

Taarifa ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imesema Uongozi umewafukuza kazi Watumishi watatu wa kivuko cha Magogoni-Kigamboni ambao ni Nahodha, Fundi wa Kivuko na Baharia kufuatia tukio lililotokea Mei 24, 2022 la kuchelewesha kwa makusudi kivuko upande wa Kigamboni na kusababisha kutokea kwa usumbufu kwa Abiria wanaotumia kivuko hicho na kuleta taharuki.

#TanzaniaWeb.Com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live