Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BWAWA LA NYERERE KUINGIZWA MAJI NOV 15

1dd04e6e54b6529dd5415aa94ac5af96.jpeg BWAWA LA NYERERE KUINGIZWA MAJI NOV 15

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Nishati , Dk Merdard Kalemani amelieleza Bunge kuwa Novemba 25, 2020 kabla ya saa 12.00 jioni maji yataanza kujazwa katika Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHP).

Dk Kalemani aliyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa miaka mitano 2021/22-2025/26 uliohitimishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Dk Kalemani aliwaeleza wabunge kuwa, Watanzania wasiwe na wasiwasi kuhusu mradi huo katika bonde la Mto Rufiji.

Alimpongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ametembelea mradi huo na kuona kwamba mradi unaendelea vizuri.

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 na utaongeza kiwango cha upatikanaji umeme nchini hadi kufikia megawati 4,887.

Dk Kalemani alisema tayari mkandarasi wa mradi huo amelipwa sh trilioni 2.04 sawa na asilimia 100 ya malipo anayotakiwa kulipwa kwa sasa, hata hivyo serikali itaendelea kumlipa kwa wakati hadi mradi utakapokamilishwa.

Alisema, serikali inazalisha umeme kwa kuzingatia vipaumbele katika kufikia uchumi wa viwanda kama nchi nyingine zinavyofanya ikiwemo China ambayo inatengeneza bwawa la kuzalisha umeme wa maji wa megawati 22,160.

Dk Kalemani alisema kwa miaka 40 hivi tangu 1964, umeme wa maji ndio ulikuwa ukitumika ukiwemo uliozalishwa Hale, Bwawa la Nyumba ya Mungu, na Mtera.

Alisema tangu miaka 2000 serikali imejikita katika umeme mchanganyiko na hadi sasa asilimia 62 ya umeme unaotumika nchini unatokana na gesi na asilimia nyingine zinatoka katika vyanzo vingine.

Alisema kati ya megawati 1,601 zinazotumika nchini, asilimia 62 unatokana na gesi.

Dk Kalemani alisema umeme wa maji ni nafuu zaidi ukifuatiwa na wa nyukilia, sola na upepo.

“Unafuata umeme wa mkaa ambayo unauzwa kwa sh 118 kwa uniti, wakati umeme wa joto ardhi unauzwa kati ya sh 119-120 kwa uniti moja na umeme wa gesi unauzwa kwa sh 147 kwa uniti moja,” alisema na kuongeza; “Umeme ambao unauzwa kwa bei kubwa ni wa mafuta mazito ambao unauzwa kwa sh 546 kwa uniti moja na ndiyo umeme wa bei kubwa zaidi kuliko mwingine wote,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz