Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azikwa baada ya kukaa siku 53 mochwari

97879 Pic+maiti Azikwa baada ya kukaa siku 53 mochwari

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Hatimaye mwili wa Kitati Nyamsacha (78) uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Nyerere wilayani hapa kwa siku 53 umezikwa baada ya Baraza la Nyumba na Ardhi Musoma kutoa kibali.

Mazishi ya Nyamsacha yamefanyika jana Jumanne, Machi 3 ndani ya kaburi lilelile alilotakiwa kuzikwa Januari 9 mwaka huu nyumbani kwake kitongoji cha Romakendo kabla ya kusitishwa na polisi kutokana na mgogoro wa ardhi uliokuwa umempa haki waliyekuwa wanashitakiana na marehemu.

Licha ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla ikiambatana na upepo na radi shughuli za mazishi ziliendelea huku baadhi wakidai kuwa ni sehemu ya baraka zake kwa wakazi wa Morotonga.

Maltha Machaba mtoto wa kaka wa marehemu amelishukuru baraza la ardhi na nyumba kuwapa kibali cha kumzika baba yao wakati kesi yao ikiendelea.

"Naomba sana wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba kunapokuwa na migogoro kama hii wahamie maeneo husika ili kupata kujua ukweli wa madai, hivyo naomba wafike huku watafikia maamzi sahihi kuhusu nani ana haki," amesema.

Fikiri Wahega mtoto wa kaka wa marehemu amesema kuwa msiba huo umewagharimu fedha nyingi kwa kuwa toka Januari 6 walianza kutoa matumizi mpaka siku ya  53 ikiwemo gharama za kuhifadhi mwili.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

"Naomba sana watu wanaohusika na utoaji haki wawe na hofu ya Mungu maana watu wengi hukata tamaa na kuacha haki zinapotea, kama ukoo tuliona haki ya marehemu baba yetu inapotea tukaamua kuisaka kwa kuchangishana, sasa ni wangapi wanauelewa huo? Alihoji.

Mchungaji wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Kisigiro Michael amewataka watu kusameheana wanapokoseana na kuwa kisasi ni kazi ya Mungu.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz