Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso kurahisisha usafiri Tanga- Zanzibar

Aweso 696x392 1.jpeg Aweso kurahisisha usafiri Tanga-Zanzibar

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso amesema atashirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah kutafuta Wadau ambao watawezesha kupatikana kwa Boat iendayo haraka (Fast Boat) ambayo itawarahisishia Watu wa Tanga, Arusha na maeneo mengine ya Kaskazini kufika Zanzibar kwa urahisi badala ya kupitia Dar es salaam.

Akiongea na Wananchi wa Pangani wakati wa Iftar aliyoiandaa ambayo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo DC wa Korogwe, jokate Mwegelo, Aweso amesema “Pangani tupo karibu na Zanzibar, leo tunaona Mtu akitoka Korogwe, Arusha, Manyara akitaka kwenda Zanzibar ni mpaka aende Dar es salaam, nikuombe DC Zainab ujenzi wa Barabara ya Tanga - Pangani - Saadan - Bagamoyo uendane na kuwaomba Wadau mbalimbali tutashirikiana kupata Fast Boat itakayokwenda Zanzibar, ili kuusaidia ukanda wa Kaskazini ili kufungua fursa za kiuchumi"

Katika hatua nyingine Aweso amesema “Mto Pangani unamwaga tu maji Baharini, ni muda sasa Mto Pangani kutumika kwa shughuli za kiuchumi, hakuna sababu nyanya za kupikia mchuzi zitoke Iringa, tulikuwa na fedha za mfuko wa Jimbo zaid ya Milioni 58 tukadema zikachochee maendeleo ya kina Mama, tukisema zigawiwe kwa vikundi kuna baadhi havitopata italeta ugomvi, niombe fedha zile zikanunue tractor kubwa lenye jembe lake ili tutumie Mto Pangani kuwekeza kwenye kilimo”

““Barabara inajengwa Tanga- Pangani - Saadani mpaka Bagamoyo tunafungua uchumi, suala la umeme Vijiji vyote vya Pangani vina umeme kimebaki kimoja tu, tulikuwa wa mwisho kielimu ila tunaongoza kwa Mkoa wa Tanga kwa mwaka wa tatu mfululizo”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live