Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso azindua mradi wa maji Muleba

Waziri Wa Maji, Juma Aweso Aweso azindua mradi wa maji Muleba

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa maji Jumaa Aweso amezindua mradi wa maji Rutenge katika Jimbo la Muleba Kaskazini unaohudumia watu zaidi ya 7000

Akikagua mradi huo, Aweso ameridhishwa na usimamizi mzuri wa meneja wa Ruwasa wilaya ya Muleba kwa kuokoa zaidi ya sh.million120 na kuagiza kiasi hicho kitumike kuwaunganishia maji wananchi majumbani.

Pia, katika jimbo la Muleba Kusini amekagua mradi wa maji Katare na kuridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya sh. bilioni 3.4 na kuagiza mradi ukamilike mwezi Oktoba mwaka huu ili wananchi wa Buganguzi wanufaike na huduma ya maji safi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live