Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso atoa wiki 6 Buswelu wapate maji - Video

Aweso Azungumzia Upungufu Wa Maji Mwanza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa wiki sita kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kukamilisha matengenezo ya upanuzi wa mtandao wa Maji Buswelu wilaya ya Ilemela Mwanza.

Waziri Aweso ameyasema hayo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Mhe Philipo Isidor Mpango ambae yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya Kikazi.

Waziri Aweso amethibitisha uwepo wa Tenki kubwa la Maji la Buswelu na kumhakikishia Makamu wa Rais ya kwamba kazi iliobaki ni usambazaji wa Maji na tayari Wizara imekwisha peleka kiasi cha Milioni Mia tano kwa Mamlaka ya Maji Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Msenyele kufanya kazi kwa haraka ndani wa wiki 6 ili wananchi wa eneo la Buswelu wapate Maji.

Katika hatua nyingine Aweso amesisitiza kuwa Mradi mkubwa wa Maji Butimba wa Chanzo cha Ziwa Victoria utakamilika mwezi Julai hivo kupelekea kuondoa changamoto ya upungufu wa upatikanaji Maji jijini Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live