Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso aridhishwa na teknolojia mradi wa maji Uvinza

Aweso Aridhishwa Na Teknolojia Mradi Wa Maji Uvinza.jpeg Aweso aridhishwa na teknolojia mradi wa maji Uvinza

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso, ametembelea mradi wa maji wa vijiji vya Mlela na Kandaga uliopo kata ya Kandaga Wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma uliogharimu jumla ya Shilingi 896,634,902.

Waziri Aweso ameipongeza RUWASA kwa kutumia teknolojia mpya ya tenki la Weholite la Lita 300,000 kwani imetumia gharama kidogo ukilinganisha na gharama za ujenzi wa tenki la zege na ujenzi umechukua muda mfupi.

Waziri wa Maji Akizungumza na wananchi wa Uvinza amesema;

“Nimefarijika sana baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Vijiji vya Mlela na Kandaga kata ya Kandaga na kujionea namna gani teknolojia ya Matenki ya Weholite inaweza kurahisisha utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa gharama nafuu na muda mfupi;

Mradi huu wa kutumia matenki haya ni matokeo ya kikao changu nilichoketi baada tu ya kuteuliwa pamoja na wenzetu wazawa wenye viwanda vinavyozalisha vifaa vya Maji na kuwashauri kuja na aina hii ya matenki ambayo yataturahisishia kupeleka huduma kwa wananchi kwa haraka na kwa gharama nafuu, niwapongeze sana wenzetu wa Plasco kwa kufanikisha hili kwa vitendo.”

Kwa upande mwingine wananchi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupata mradi huo ambao umetatua kero ya maji katika vijiji hivyo na kumtua mama ndoo kichwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live