Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso aridhia kuanzishwa kwa mamlaka ya maji Songwe

Aweso Azungumzia Upungufu Wa Maji Mwanza Aweso aridhia kuanzishwa kwa mamlaka ya maji Songwe

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema Katika kuhakikisha adhma ya kumtua ndoo Mama kichawani inafikiwa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa asilimia 95 mijini na asilimi 85 vijijini ifikapo 2025 ni vema kuyafikia maeneo yenye changamoto na kuzitatua.

Aidha Waziri Aweso akiwa wilayani Songwe amezindua mradi wa Maji wa Saza eneo ambalo lilikua na changamoto kubwa ya Maji ambapo wananchi wameupokea mradi huo kwa shangwe wakiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa Utekelezaji huu.

Akizungumza na wakazi wa wilaya ya Songwe alipokua akihitimisha Ziara yake Wilayani humo katika mkutano wa hadhara Waziri wa Maji,Jumaa Aweso ameridhia ombi la Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philipo Mlugo la kuanzisha mamlaka ya maji itakayohudumia eneo la mjini kwani kuna ongezeko kubwa la watu kutokana na ukuaji mkubwa wa uchumi hususani uchimbaji wa madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live