Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso anavyohangaika kumtua mama ndoo kichwani Tanzania

91156 Pic+awesu Aweso anavyohangaika kumtua mama ndoo kichwani Tanzania

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Itilima. Naibu Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amewaagiza watalaam wa maji kutoka wizara hiyo na wale wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha miradi ya maji inakamilika kwa wakati.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa maiji wa Nkoma Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu huo jana Jumanne Januari 7, 2020, Aweso alisema hajaridhishwa na utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh1.3 bilioni ambao haujakamilika tangu mwaka 2014.

Kutokana na kusuasua kwa mradi huo, Aweso aliwaagiza wataalam wa maji kutoka wizarani, Mamlaka ya Bonde la Ziwa Victoria na mkandarasi anayetekeleza mradi huo  kukutana naye leo Jumatano Januari 8, 2020 saa mbili asubuhi kupanga mikakati ya kukamilisha mradi huo.

"Mkandarasi hana kisingizio cha kuchelewesha mradi kwa sababu Serikali imeshamlipa zaidi ya 331 milioni; Wanachotaka wananchi ni maji kwenye mabomba yao. Mkandarasi lazima aongeze vifaa na nguvu kazi," alisema Aweso

Naibu Waziri huyo pia alimwagiza meneja wa Ruwasa Wilaya ya Itilima,  Banda Issa kuongeza usimamizi kuhakikisha mkandarasi kutoka kampuni ya Best One Limited ya Dar es Salaam anakamilisha mradi huo kabla mwezi Machi mwaka huu.

"Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huu," alisema

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, meneja wa Ruwasa Wilaya ya Itimila,  Banda Issa alisema tayari matenki mawili yenye ujazo wa tani 135, 000 yamejengwa huku tenki lingine na vituo 22 vya kuchotea maji ikiendelea kukarabatiwa.

 

"Kazi ya ujenzi wa chujio, utandazaji wa mabomba kwenye eneo la kilomita 33.3 ununuzi wa pampu na ujenzi wa nguzo za umeme kuunganisha chanzo cha maji katika bwawa la Nkoma inaendelea," alisema Issa

Katika taarifa yake, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi alimweleza Aweso kuwa kusuasua kwa mradi huo kunafifisha matumaini ya wananchi ya kupata maji safi na salama.

"Moja ya changamoto kubwa kwa Wilaya ya Itilima ni ukosefu wa vyanzo vya asili vya maji kama mito na chemichemi. Tunategemea visima na mabwawa ndiyo maana uongozi wa wilaya unafuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maji inayosuasua lucha ya Serikali imetoa mamilioni ya fedha," alisema Kilangi

Chanzo: mwananchi.co.tz