Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso amsimamisha kazi Kaimu Meneja wa Ruwasa

AWESO AKAMATA Aweso amsimamisha kazi Kaimu Meneja wa Ruwasa

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Kaimu Meneja Ruwasa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Bakari Kiwitu na kumuondoa katika mradi Mkandarasi Nangai Engineering na Contractors wa mradi wa maji Kazuramimba kwa kushindwa kukamilisha ujenzi huo.

Kwenye eneo la tukio Waziri aweso alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinah Mathamani kuwaweka chini ya ulinzi Mafundi sanifu hawa wa mradi kwa sababu walisema mabomba yanafanya kazi kitu ambacho hakikuwa kweli kwani walimembeza Waziri kilometa zote tatu na hakuna bomba lililotoa maji.

Kitendo cha Waziri kutembezwa kwa umbali mrefu bila ya mafanikio baadhi ya Wananchi walichukizwa kuona Waziri amesumbuliwa bure na kuwafanya waanzishe vurugu na kutaka kumpiga Fundi sanifu wa mradi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live