Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso aeleza mikakati ya upatikanaji maji Longido

Aweso Pc Data.png Waziri wa Maji, Juma Aweso

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema watendaji wa wizara hiyo hawatakuwa kikwazo kwa Watanzania kupata maji safi na salama na ya kutosheleza.

Waziri huyo ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 18, 2021 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji Longido, Arusha.

Waziri huyo amemshukuru Rais Samia kwa niaba ya watendaji wa wizara hiyo kwa kuendelea kuwaamini viongozi wa kuu katika sekta hiyo, akijitolea mfano mwenyewe kwamba tangu alipomaliza chuo kikuu kazi yake ya kwanza ni Ubunge.

“Sikuwahi kufanya kazi popote lakini wewe na Hayati John Magufuli mliniamini kuwa Naibu Waziri wa Maji na leo Waziri wa Maji sio jambo jepesi, familia yangu mama yetu ni mama ntilie kabisa lakini umeniamini na kunipa dhamana hii kubwa,” amesema

Amesema wakati anateuliwa, Rais Samia alimuita Ofisi kwake na kumueleza baadhi ya mambo ikiwemo kumsikiliza na kumuelewa kwamba sehemu zote alizopita changamoto kubwa aliyokutana nayo ni maji.

“Waathirika wakubwa ni akina mama na wanatembea umbali mrefu, wakati huo baba wamemuacha nyumbani akihitaji maji na kuoga lakini hawajuhi maji yanapatikana wapi na ndoa nyingi zinateteleka kwa sababu ya ukosefu wa maji,” amesema Aweso.

Waziri huyo amemueleza Rais Samia utekelezaji wa miradi unategemeana na fedha na anaishukuru serikali imekuwa ikitoa fedha kuhakikisha miradi yote inakamilika.

Amesema mradi huo wa Longido umetekelezwa kwa Sh15.8 bilioni fedha hizo ni za ndani ambazo wananchi wamekuwa wakilipa kodi na wala sio za mkopo.

Chanzo: mwananchidigital